1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Sunak kuimarisha mpango wake wa kuwapeleka wahamiaji Rwanda

Tatu Karema
14 Desemba 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema yuko tayari kuuimarisha mpango wake wenye utata wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda ambao umekigawa chama chake tawala cha Conservative.

https://p.dw.com/p/4aADU
Uingereza | Waziri Mkuu Rishi Sunak
Waziri Mkuu Rishi SunakPicha: Henry Nicholls/AFP/Getty Images

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amewaambia wanahabari kwamba mara kwa mara amekuwa wazi kama walivyokuwa mawaziri wote kwamba kama kuna njia ambazo sheria hiyo inaweza kuboreshwa na kudumisha ushiriki wa Wanyarwanda katika mpango huo, bila shaka wanaweza kuzingatia hilo.

Mswada huo wa dharura na uliochapishwa wiki iliyopita, ni jibu la Sunak kwa uamuzi wa mahakama ya juu kwamba sera iliyotumia ilikuwa kinyume cha sheria.

Mswada huo utakapopitishwa, utawalazimisha majaji kuichukulia Rwanda kama nchi ya tatu salama na pia unapendekeza kuwapa mawaziri wa Uingereza mamlaka ya kupuuza sehemu za sheria za kimataifa na Uingereza za haki za binadamu.