1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiLebanon

Hezbollah yahimiza kuruhusu boti za wahamiaji kuelekea Ulaya

14 Mei 2024

Hassan Nasrallah ameihimiza mamlaka ya Lebanon kuruhusu boti za wahamiaji kuelekea Ulaya katikati ya ongezeko la chuki dhidi ya Syria na madai kuwa mataifa ya Magharibi yanataka wakimbizi wabakie nchini Lebanon.

https://p.dw.com/p/4fokF
Raia wa Syria waliokimbia vita nchini mwao
Raia wa Syria waliokimbia vita nchini mwaoPicha: Bakr Alkasem/AFP/Getty Images

Katika hotuba ya televisheni, kiongozi huyo wa Hezbollah ametoa wito kwa mamlaka kufungua njia ya bahari na kuruhusu yeyote anayetaka kwenda Ulaya kwa boti kufanya hivyo.

Hata hivyo, ameeleza kuwa hawalazimishi raia wa Syria waliokimbia makwao kupanda boti na kuelekea Cyprus au nchi nyengine za Ulaya.

Soma pia: Jenerali wa zamani wa Syria kushtakiwa Sweden kwa uhalifu wa kivita

Matamshi yake ameyatoa kama sehemu ya kuushinikiza Umoja wa Ulaya baada ya umoja huo kutangaza mapema mwezi huu msaada wa dola bilioni 1 kwa Lebanon ili kusaidia kukabiliana na wimbi la wahamiaji.

Cyprus, nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya iliyo upande wa mashariki, iko chini ya kilomita 200 kutoka Lebanon na Syria na inataka kuzuia kuondoka kwa boti za wahamiaji kuelekea pwani yake.