1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIran

Meli ya kivita ya Iran yavuka Ikweta hadi Kizio cha Kusini

Saleh Mwanamilongo
4 Mei 2024

Iran yasema Meli yake kivita iitwayo Shahid Mahdawi, ikiwa na droni na makombora, kwa mara ya kwanza, imevuka Ikweta hadi Kizio cha Kusini.

https://p.dw.com/p/4fVlV
Iliyokuwa meli ya makontena ya Iran yageuzwa meli ya kivita
Iliyokuwa meli ya makontena ya Iran yageuzwa meli ya kivitaPicha: Jon Gambrell/AP Photo/picture alliance

Taarifa hiyo imetolewa na redio ya taifa ya Iran, ambayo, hata hivyo, haikufafanua kuhusu mahali halisi inapopatikana meli hiyo.

Shahid Mahdawi ni meli iliyogeuzwa kutoka meli ya kubeba makontena na kuwa meli ya kivita. Na inaendeshwana  wanajeshi wa kitengo maalum cha Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Kikosi hicho kilizinduliwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Kwa mara ya kwanza, mwezi Februari, vikosi vya Iran viliyafanyia majaribio makombora ya masafa ya kati yenye uwezo wa kufikia umbali wa karibu kilomita 1,700.