1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Kimbunga Hidaya chasababisha Kenya kuahirisha kufungua shule

Lilian Mtono
3 Mei 2024

Rais wa Kenya William Ruto ameahirisha mpango wa kuzifungua tena shule wiki ijayo hadi kutakapotolewa tangazo jingine, wakati mvua kubwa na mafuriko yaliyowaua watu zaidi ya 200 yakiendelea.

https://p.dw.com/p/4fURU
Kenya Nairobi | William Ruto
Rais William Ruto wa Kenya Picha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Rais Ruto amesema kwenye hotuba yake ya hali ya taifa hii leo kwamba ripoti za mamlaka za hali ya hewa zinaibua wasiwasi, huku akikiangazia Kimbunga Hidaya kinachotarajia kuipiga pwani ya Kenya siku zijazo.

Mamlaka za hali ya hewa zimetahadharisha kwamba Kenya itakumbwa na kimbunga cha kwanza kabisa kinachoitwa Hidaya na kusababisha mvua kubwa, upepo mkali na mawimbi makubwa na kuathiri shughuli za baharini na makazi ya eneo la pwani. taifa letu linatakiwa kuchukua hatua madhubuti za kuyakabili maafa na kulinda maisha ya watu na mali.

Kenya, Tanzania zakabiliwa na kimbunga Hidaya

Kenya na mataifa mengine ya Afrika Mashariki yameelemewa na mafuriko, na sasa zaidi ya watu 150,000 wanaishi kwenye makambi baada ya kulazimika kuyakimbia makaazi yao.