1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani ya Kusini

Colombia yafikia makubaliano ya usitishaji mapigano na waasi

3 Septemba 2023

Serikali ya Colombia imefikia mwafaka wa kurejesha makubaliano ya usitishaji mapigano na mazungumzo ya amani na kundi la wapiganaji wa msituni la EMC.

https://p.dw.com/p/4VtWy
Wapiganaji wa kundi lililosambaratishwa Colombia, FARC
Wapiganaji wa kundi lililosambaratishwa Colombia, FARCPicha: JOAQUIN SARMIENTO/AFP

Makubaliano hayo yamevunjika mara kadhaa katika miezi ya hivi karibuni. Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za rais wa mrengo wa kushoto Gustavo Petro kupanua mapatano ya amani ya mtangulizi wake na kundi kubwa la waasi nchini humo, FARC, ambalo liliweka silaha chini mwaka 2016. Taarifa ya pamoja iliyotolewa inasema makubaliano ya sasa yanalenga kupunguza makabiliano na vurugu.

Soma zaidi: Ugomvi wa Colombia na wanamgambo wa FARC umekwisha

Usitishaji huo wa mapigano utatumika kote nchini kwa lengo la kuyajumuisha mashirika ya kiraia katika mchakato wa amani. EMC ni kundi la wapiganaji wa msituni, ambalo lilijitenga na kundi FARC na kukataa mazungumzo ya amani na serikali ya Colombia yaliyoanza 2016 na kuendeleza uhasama.