1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yapinga azimio la UN la kuzuia silaha za nyuklia

Tatu Karema
25 Aprili 2024

Urusi jana ilipinga azimio la Umoja wa Mataifa lililowasilishwa na Marekani na Japan linalotaka mataifa yote kuzuia matumizi ya silaha za nyuklia katika anga za mbali.

https://p.dw.com/p/4fBhe
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa NewYork
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa NewYorkPicha: Loey Felipe/UN Photo/Xinhua/picture alliance

Nchi 13 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ziliunga mkono azimio hilo huku Urusi ikitumia kura yake ya turufu dhidi ya azimio hilo na China haikupiga kura.

Baada ya kura hiyo, Balozi wa Marekani kwenye Umoja huo Linda Thomas-Greenfield, alisema Rais wa Urusi Vladimir Putin aliarifu kwamba nchi yake haina nia ya kupeleka silaha za nyuklia katika anga za mbali lakini hatua ya kupinga azimio hilo inaibua swali juu ya dhamira iliyojificha ya serikali ya nchi hiyo.

Azimio hilo lilikuwa linatoa wito kwa nchi zote kutotengeneza ama kupeleka silaha za nyuklia ama silaha nyingine za maangamizi makubwa angani, kama ilivyopigwa marufuku chini ya mkataba wa kimataifa wa 1967 uliozijumuisha Marekani na Urusi , na kukubaliana kuhusu hitaji la kuthibitisha utiifu.