1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan Kusini

Malori ya msaada wa kibinadamu yakwama kwenye mpaka wa Sudan

Tatu Karema
25 Aprili 2024

Umoja wa mataifa wasema malori yanayosafirisha bidhaa za misaada ya kibinadamu zinazohitajika kwa kiasi kikubwa nchini Sudan Kusini, yamekwama kwenye mabohari na kivuko cha mpaka kutokana na mzozo wa kodi.

https://p.dw.com/p/4fBhf
Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini
Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan KusiniPicha: picture alliance/Yonhap

Wiki hii, wizara ya biashara nchini humo ilianzisha ushuru mpya wa dola 300 kwa kila lori linalosafirisha bidhaa ndani au nje ya nchi hiyo inapotafuta kuongeza mapato.

UNMISS imesema kutokana na hatua hiyo, serikali ilikuwa bado haijatoa kibali cha kuvuka kwa malori hayo yaliokodishwa na Umoja huo wa Mataifa yaliyokuwa yamepakia mafuta kutoka nje licha ya kuhakikishiwa kuwa yamesamehewa kulipa kodi.

Kaimu msemaji wa UNMISS Priyanka Chowdhury, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanaendelea kufanya mashauriano na maafisa wa ngazi za juu ili kutatua suala hilo.

Misheni za kidiplomasia zimepinga hatua hiyo, huku zikitoa wito wa kuondolewa kwa ushuru huo dhidi ya mashirika ya kibinadamu.